InshaKuna aina mbili kuu za Insha.Insha za ubunifuInsha

Insha

Kuna aina mbili kuu za Insha.

  1. Insha za ubunifu
  2. Insha za kiuamilifu

Insha za ubunifu ni insha ambazo mwanafunzi huhitaji kubuni maudhui, mazingira, wahusika, na kadhalika kulingana na swali analorejelea. Insha hizi zinaweza kuwa za methali, mdokezo ama insha zenye mada ambazo hazina mtindo rasmi.

Insha za kiuamilifu ni maandishi yenye mtindo maalum na hutumika katika mazingira halisi kwa kuzingatia mtindo huo rasmi. Kwa mfano kumbukumbu, resipe, barua, ratiba, n.k. Ubunifu wa mwanafunzi hauwezi ukaathiri mtindo wa insha hizi. Kwa hivyo anchohitajika zaidi kuzingatia ni mtindo wa utunzi mada na hoja muhimu.

Insha za Kubuni

Aina za Insha za Kubuni

  1. Insha za Mdokezo
  2. Insha za Methali
  3. Insha za Mada

Insha za Mdokezo

InshaZa Kubuni • Insha za Mdokezo

Hizi ni Insha za ubunifu ambazo mwanafunzi hupewa kifungu cha maneno kinachopaswa kujitokeza katika insha yake.

Baadhi ya insha za aina hii huwa zimetangulizwa na mwanafunzi hutakiwa akamilishe na nyinginezo huwa na kimalizio. Japo mwanafunzi ana uhuru wa kuiendeleza insha yake atakavyo, ni sharti ajifunge katika maudhui yanayojitokeza katika mdokezo aliopewa. Kwa hivyo, kabla ya mwanafunzi kuiendeleza insha yake, ni sharti atambue maudhui yaliyokusudiwa na mtahini.

Kwa mfano:

Endeleza insha ifuatayo na uifanye iwe ya kuvutia:

  1. Nikasikia sauti hiyo tena. Sikuamini masikio yangu. Moyo ukaanza kunienda mbio mbio. Mara upepo….
  2. Giza lilikuwa limechukua milki ya viumbe wote duniani. Nyota zilitoa mwanga hafifu na mwezi ulikuwa ushatua. Katika giza hilo la kaniki….

au

Andika insha inayoishia kwa dondoo hili…

  1. … na kuniacha machozi yakinienda mbilimbili.
  2. … Hadi wa leo, juhudi zangu za kusahau matukio ya siku hiyo hazifui dafu.

Insha za Methali

InshaZa Kubuni • Insha za Methali

Methali huwa na pande mbili na ni lazima insha ya methali izipe sehemu zote mbili uzito sawa. Upande mmoja hutoa wazo au pendekezo; na upande wa pili hutoa jibu, suluhisho au matokeo.

Chukua kwa mfano, “Mpanda ngazi hushuka“. Katika insha yako ni lazima utoe hoja za kutosha kuonyesha kwamba mhusika fulani kweli alipanda ngazi (k.v alipata cheo kikubwa, alijisifu n.k). Mwandishi pia anapaswa kutoa hoja za kutosha kuonyesha namna mhusika huyo aliposhuka (k.v akafutwa kazi,n.k) . Kwa mara nyingi, wanafunzi huzingatia tu sehemu ya kwanza ya methali katika insha yote huku sehemu ya pili ikijitokeza katika aya ya mwisho pekee.

Kumbuka kwamba ni muhimu kuelewa maana ya methali vizuri kabla ya kuchagua insha ya methali.

Mifano ya Insha za Methali:

Andika inayoonyesha ukweli wa methali ifuatayo. Ifanye insha yako iwe ya kupendeza.

  1. “Usiache mbachao kwa msala upitao”
  2. “Chururu si ndo ndo ndo”
  3. “Siku za Mwizi ni arobaini”

Insha za Mada

InshaZa Kubuni • Insha za Mada

Hizi ni insha ambazo mwaandishi hutakiwa kuzungumzia mada fulani kwa kutoa hoja ama maelezo. Insha hizi hazimhitaji mtahiniwa kuanza kusimulia hadithi yake bali ni kurejelea mada aliyopewa. Mwandishi wa insha kama hii anapaswa kuwa na hoja za kutosha kuhusu mada aliyopewa kabla ya kuanza kuiandika. Hoja zote zinapaswa kujitokeza katika masimulizi yenye mtiririko wala si kuorodhesha hoja, moja baada ya jingine.

Kwa mfano:

Andika insha juu ya:

  1. Umuhimu wa kupanda miti
  2. Athari za kuavya mimba
  3. Namna ya kuboresha kilimo katika sehemu zenye ukame
  4. Mbinu za kukabiliana na wezi wa mifugo.

Insha hizi huwa insha halisia na hivyo mwaandishi hawezi kupigia chuku au kutoa hoja zisizo kweli. Kwa mara nyingi insha hizi hurejelea maswala ibuka katika jamii k.v njaa, ukimwi, kilimo, ufisadi, ukabila, n.k

Hata hivyo mwanafunzi anaweza kupata insha za mada zinazohitaji ubunifu, mapambo ya lugha n.k. Angalia mifano ifuatayo.

Andika insha juu ya:

  1. “Ndoto Niliyokuwa Nayo”
  2. “Siku Ambayo Sitaisahau Maishani”
  3. “Sherehe Niliyoihudhuria”
  4. “Ajali ya Barabarani Niliyoishuhudia”

Insha za Barua

InshaZa Kiuamilifu • Insha za Barua

Kuna aina mbili za barua:

  • Barua Rasmi
  • Barua ya Kirafiki

Pia tutaangalia Barua Kwa Mhariri

Barua ya kirafiki

Barua ya kirafiki ni barua ambayo mtu huandika kwa mwenzake au mtu wa familia yake. Barua hii haichukui mtindo wowote maalum wa kuandikwa. Huwa na anuani moja tu: ya mpokeaji. Barua hii haitumii lugha rasmi na mwandishi anaweza kumrejelea mwandikiwa kwa kutumia jina lake la kwanza. Aidha barua za kirafiki haziitaji kutiwa saini.

Barua Rasmi

Barua rasmi au barua ya kiofisi/kibiashara huzingatia mtindo rasmi wa barua. Huwa na sehemu zifuatazo:

Muundo

  1. Anuwani ya mwaandishi huwekwa juu kabisa na huwa katika upande wa kulia wa kartasi.
  2. Tarehe ya barua hiyo – tarehe huandikwa chini ya anwani ya mwandishi
  3. Anuwani ya mpokeaji – Anwani ya anayeandikiwa huwa katika upande wa kushoto wa kartasi, na huwekwa msitari mmoja chini ya tarehe.
  4. Salamu-Chini ya anwani ya mpokeaji, barua huanza kwa kumrejelea mpokeaji kama bwana au bi. Ni makosa kumsalimia mpokeaji wa barua rasmi au kumwuliza hali yake.

Kwa Bwana Menomakubwa, => taja jina lake ikiwa mnajuana na unayemwandikia.
Kwa Bw/Bi, => Ikiwa humjui mpokeaji wa barua, tumia bw/bi

  1. Mada -Kichwa cha barua rasmi huja pindi tu baada ya salamu. Hutangulizwa na maneno kama vile KUH:(kuhusu), MINT:(mintarafu). Ni sharti kiachwe kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe mstari. Kichwa kinapaswa kuwa kifupi na kinachoelezea mada ya barua kiukamilifu.
  2. Ujumbe – Ujumbe wa barua rasmi lazima uwe mfupi na unaotumia lugha rasmi.
  3. Tamati – mwandishi humalizia kwa maneno ya hitimisho kama vile:

Wako mwaminifu,

[jina]

Sahihi

Barua kwa Mhariri

Hii ni barua ya msomaji wa jarida kwa mhariri mkuu wa jarida/gazeti fulani akitoa maoni yake kuhusu jambo fulani kama vile uchumi, kisa, sera za serikali au habari zozote zinazoendelea kwa wakati huo.

k.m:

Kwa Mhariri Mkuu

Jarida la Mwenda Zake Leo

MINT : HATUA YA SERIKALI KUFADHILI SEKTA YA BODABODA

…ujumbe…

Na [jina]

Hotuba

InshaZa Kiuamilifu • Hotuba

Insha ya hotuba ni insha ambayo hutoa maneno halisi ya mzungumzaji/hatibu/kiongozi anapozungumzia hadhira, kuhusu jambo fulani. Insha ya hotuba huandikwa katika hali ya usemi halisi na mwandishi hatakiwi kuweka alama za kunukuu anapoanza insha yake.

Hotuba inaweza kutolewa na kiongozi wa kisiasa, utawala, kidini, kikundi, shirika fulani, daktari, n.k. Hadhira katika hotuba husheheni wageni waalikwa, wanachama, wafuasi, wananchi, n.k ambao wanahusishwa katika mada inayorejelewa katika hotuba hiyo. Mengi ya maswala yanayojitokeza katika insha za hotuba ni maswala ibuka katika jamii k.v upangaji wa uzazi, usalama, n.k

Muundo wa Hotuba

1.      Anwani

Anwani, mada au kichwa cha hotuba huchukua herejelea hatibu pamoja na mada ya hotuba. Pia mada inaweza kutaja hadhira.

    • Hotuba ya Waziri wa Afya kuhusu madhara ya ukimwi kwa wananchi.
    • Hotuba ya Mwalimu Mkuu kwa Wazazi

2.      Utangulizi

    • Anza hotuba yako kwa kuwatambua waliohudhuria mkutano (hadhira).
    • Wataje kwa majina/vyeo vyao kuanzia yule wa cheo cha juu hadi wa chini, mabibi na mabwana. Kumbuka kwamba hauhitajiki kuwasalimia. Kuwatambua kwa majina pekee kunatosha.
    • Jitambulishe kwa hadhira yako hasa ikiwa unazungumzia hadhira isiyokujua au wageni.
    • Tanguliza mada yako. Kwa mfano:

Waziri wa Kilimo, Mkuu wa Wilaya, Chifu wa Kisioni, wanachama wa kikundi hiki cha Rotuba Bora, mabibi na mabwana. Ni matumaini yangu kwamba nyote mu buheri wa afya. Mimi ni mwakilishi wa Kikundi cha Mshipi wa Kijani Kibichi na jioni ya leo kuna jambo muhimu ambalo ningependa sote tulifahamu ili kuboresha mazingira yetu kwa …

3.      Mwili

    • Hakikisha kuna mtiririko wa hoja kuanzia mwanzo hadi mwisho
    • Ujumbe wako wote unapaswa kuwa katika usemi halisia wala si wa taarifa.

4.      Tamati

    • Hakikisha kwamba mwisho wa hotuba yako unatambulika.
    • Unaweza kumaliza kwa shukurani

Mfano ya Insha za Hotuba:

  1. Wewe ni chifu katika kijiji cha Kikanyageni. Andika hotuba utakayotoa kwa vijana kuhusu hatua za serikali kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya.
  2. Umealikwa kuwahutubia wanafunzi wa shule ya msingi uliyosomea kuhusu umuhimu wa elimu ya wasichana. Andika hotuba utakayotoa.
  3. Wewe ni daktari. Andika hotuba utakayotoa kuwahimiza wanawake wakubali kutumia mbinu za kupanga uzazi.
  4. Umeteuliwa na afisa katika idara ya utalii kuhutubia watalii kuhusu changamoto za kiusalama zinazolikabili bara hili na upendekeze mbinu za kuzitatua.

nsha za Kumbukumbu

InshaZa Kiuamilifu • Insha za Kumbukumbu

Kumbukumbu za mikutano ni rekodi zinazowekwa na katibu wa mkutano mkutano unapoendelea ili kuhifadhi yanayojadiliwa na kukubalianwa katika mkutano huo. Katibu anapaswa kufuatilia mtindo maalum wa kuandika kumbukumbu hizo kulingana na mpangilio katika mkutano.

Muundo wa Kumbukumbu

  1. Kichwa cha kumbukumbu – Kichwa cha kumbukumbu kinapaswa kutaja mambo yafuatayo:
    • Ni mkutano wa akina nani?
    • Unaandaliwa wapi?
    • Unaandaliwa lini?
    • Unaanza saa ngapi?

Mfano wa Kichwa cha Kumbukumbu:

Kumbukumbu za Mkutano wa Shirika la Msalaba Mwekundu Shuleni ulioandaliwa tarehe saba Agosti 2001 katika Ukumbi wa Mikutano kuanzia saa Tisa alasiri.

  1. Waliohudhuria – Andika orodha ya wote waliofika kwenye mkutano huku kuanzia na yule mwenye cheo cha juu zaidi hadi kwa wanachama. Pia onyesha vyeo vyao.
  2. Waliotoa Udhuru -Hawa ni wale walioomba ruhusa kutohudhuria mkutano
  3. Waliokosa kuhudhuria -Hawa ni waliokosa kuhudhuria mkutano, bila kutoa udhuru)
  4. Waalikwa – Hawa ni wageni walioalikwa katika mkutano, k.v mlezi wa chama, afisa wa kiutawala, n.k)
  5. Ajenda orodhesha hoja zitakazorejelewa katika mkutano huo

KUMB 1

kumbukumbu ya kwanza huwa ni kufunguliwa kwa mkutano na ujumbe kutoka kwa mwenyekiti.

KUMB 2

Kusomwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia na kuthibitishwa kwa kumbu kumbu hizo kwa kutiwa saini.

KUMB 3

Maswala yanayoibuka kutokana na kumbu kumbu zilizosomwa. (Kumbuka kutaja nambari ya kumbu kumbu hizo)

KUMB 4 kuendelea

Maswala katika ajenda

KUMB ya Mwisho

Maswala mengineyo yasiyokuwa kwenye orodha ya ajenda.

Tamati

kufungwa kwa mkutano. Taja mkutano ulifungwa saa ngapi; mkutano ujao utakuwa tarehe ngapi; kisha acha nafasi ya kuthibitishwa kwa kumbu kumbu hizo katika mkutano utakaofuatia.

Mfano wa Insha ya Kumbukumbu

KUMBUKUMBU ZA MKUTANO WA CHAMA CHA KISWAHILI ULIOANDALIWA KATIKA CHUMBA CHA MIJADALA TAREHE 2 APRILI 2010 KUANZIA SAA TATU ASUBUHI

Waliohudhuria

  1. Thoma Mwororo – Mwenyekiti
  2. Vivian Mjaliwa – Mweka hazina
  3. Idi Baraka – Mkuu wa utafiti
  4. Fikra Mawimbi – mwanachama
  5. Mercy Rehema – katibu

Waliotuma Udhuru

  1. Bahati Sudi – Naibu Mwenyekiti
  2. Paul Kitanzi – Msimamizi wa Mijadala

Waliokosa Kuhudhuria

  1. Zakayo Chereko – Spika
  2. Juma Mtashi – mwanachama

Waalikwa

  1. Mdaku Mpelelezi – Mwanahabari
  2. Bw. Msawali – Mlezi wa Chama.

Ajenda

  1. Uchapishaji wa jarida la Kiswahili
  2. Shindano la kuandika insha.
  3. Kusajili wanachama wapya

KUMBUKUMBU 1/04/10 – KUFUNGULIWA KWA MKUTANO

Mwenyekiti aliwakaribisha wanachama wote na baada ya kuwatambulisha wageni, akawaomba washiriki wawe huru kuchangia katika ajenda mkutano huu ili kuboresha chama.

KUMBUKUMBU 2/04/10 – KUREJELEA KUMBUKUMBU ZA MKUTANO ULIOPITA.

Katibu alisoma kumbukumbu za mkutano wa mwezi Machi. Kumbukumbu zilikubaliwa na wanachama wote na kuthibitishwa na mwewnyekiti pamoja na katibu kwa kutia saini.

KUMBUKUMBU 3/04/10 – MASWALA IBUKA KUTOKANA NA KUMBUKUMBU ZILIZOSOMWA

Mweka hazina alifahamisha mkutano kwamba aliongea na mkuu wa idara ya Kiswahili kuhusu ufadhili kama tulivyokuwa tumekubaliana katika KUMB 9/03/10 ya mkutano uliopita.

KUMBUKUMBU 5/04/10 – HAFLA YA KISWAHILI

Iliripotiwa kwamba hafla ya Kiswahili ambayo wanachama walikuwa wamealikwa kuhudhuria katika Shule ya Sakata Academy haingeweza kufanyika kutokana na tamasha za muziki zilizokuwa zinaendelea katika shule hiyo. Wanachama waliokuwa wamejitayarisha kwa mashairi waliombwa kuendelea kujifunza ili wayawasilishe muhula wa pili.

KUMBUKUMBU 4/04/10 – UCHAPISHAJI WA JARIDA LA KISWAHILI

Wanachama walikubaliana:-

  • Kwamba chama kitaanza kuchapisha jarida la Kiswahili
  • Kwamba jarida litakuwa likichapishwa mara moja kila muhula na kuuzwa shuleni
  • Kwamba kila mwanachama atachangia katika kuandika makala na kuuza nakala za jarida hilo.
  • Kwamba paneli ya wahariri lingeundwa ili kuongoza idara ya uchapishaji
  • Kwamba hazina ya chama ina fedha za kutosha kuzindua uchapishaji huo.

KUMBUKUMBU 5/04/10 – SHINDANO LA KUANDIKA INSHA

Kila muhula wa pili, chama huandaa shindano la kuandika insha ambalo wanafunzi wote hushiriki. Insha zilizopendekezwa mwaka huu ni:-

  • “Jadili chanzo cha migomo shuleni na namna ya kusuluhisha.”
  • … … … … … … … … …
  • … … … … … … … … …
  • … … … … … … … … …

KUMBUKUMBU 6/04/10 KUSAJILI WANACHAMA WAPYA

… … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …

KUMBUKUMBU 7/04/10 MASWALA MENFINEYO

… … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …

KUFUNGWA KWA MKUTANO

Mkutano ulifungwa saa kumi na nusu, baada ya maswala yote kujadiliwa. Mkutano unaofuatia ulipoangwa kuwa tarehe ishirini mwezi Mei, katika Ukumbi wa Muziki.

KUTHIBITISHWA KWA KUMBU KUMBU

______________

_____________

Mwenyekiti

Katibu

Tarehe:________

Tarehe:________

Tanbihi: Usitie saini. Sahihi itawekwa katika mkutano ufuatao

Insha za Mazungumzo au Majadiliano

InshaZa Kiuamilifu • Insha za Mazungumzo au Majadiliano

Hii ni insha ya mazungumzo baina ya watu wawili au zaidi. Ni lazima wahusika katika mazungumzo wajitokeze vizuri na sifa zao zitambulike. Hatutarajii watu katika mazungumzo wawe na fikira moja na usawa katika mapendekezo yao. Ukinzani au tofauti ya uteuzi wa maneno kati ya usemi wa mzungumzaji mmoja na mwengine ni lazima ijitokeze.

Mazungumzo yanaweza kuwa ya kutafuta suluhisho baina ya pande mbili zinazozozana kama vile mama na bintiye; kupanga jambo fulani, n.k

Insha ya Mazungumzo huandikwa katika usemi halisia, huku wasemaji wakionyeshwa kama vile mchezo wa kuigiza.

Vitendo vya wahusika huonyeshwa kwa mabano

Mfano wa Insha ya Mazungumzo

Mazungumzo baina ya Mwalimu Mkuu, Mwanafunzi na Babake kuhusu nidhamu ya mwanafunzi huyo.

Mwalimu:

Bwana Juma, nimekuita umchukue mtoto wako ukamsomeshe katika shule nyingine kwa maana amtushinda sisi.

Mzazi:

Ikiwa amewashinda na ninyi ndio mlio na kiboko, si ataniua mimi! Hata mimi simtaki kwa maana simwezi. Hawezi kuja kwangu

Juma:

Nimesema sitaki kusoma! Nimechosha na mtindo huu…

Mzazi:

(akikunja shati)… …

nsha za Mjadala

InshaZa Kiuamilifu • Insha za Mjadala

Insha ya mjadala humhitaji mwanafunzi atoe maoni yake kuunga mada na pia kupinga kauli fulani. Katika insha za aina hii, mwanafunzi anaweza kuegemea upande mmoja tu ikiwa upande wa kupinga hauna hoja za kutosha.

Ratiba

InshaZa Kiuamilifu • Ratiba

Ratiba ni orodha ya mpangilio wa namna mambo yatakavyofuatana katika shughuli fulani. Lengo lake ni kuhakikisha wakati unatumiwa vizuri ili mambo fulani yasije yakakosa kutendwa kutokana na upungufu wa wakati.

Ratiba hutumika katika sherehe, mikutano, mazishi, hafla, tamasha, n.k

Sehemu za Ratiba

1.      Kichwa

Kichwa cha ratiba hutaja mambo yafuatayo:

    1. Shughuli yenyewe – Taja jina la tukio ambalo unaandalia ratiba. Kwa mfano Harusi ya Bwana na Bi Arusi, Siku ya Zawadi
    2. Tarehe ya shughuli – je shughuli hiyo itafanyika lini?
    3. Mahali- Taja mahali ambapo shughuli hiyo itafanyikia. kwa mfano katika uwanja wa michezo wa Kasarani, kanisa la St. Mtakatifu

Mfano wa kichwa cha ratiba:

  • Ratiba ya Hafla ya Ukimwi katika Bustani la Uhuru tarehe tano Januari.
  • Ratiba ya Mazishi ya Dkt. Marehemu tarehe 20/12/1923 Kijijini Vikwazoni

                        Mwili

Mwili wa ratiba hujumuisha mambo mbalimbali yatakayofanyika katika mpangilio maalum, saa mbalimbali. Ni vizuri kuzingatia vipengele vifuatavyo:

  1. Saa – Onyesha saa ambazo tukio limepangiwa kuanza hadi linapotakiwa kumalizika
  2. Mahali – Ikiwa shughuli tofauti zinafanyika katika mahali mbalimbali kama vile vyumba tofauti, inapaswa hutaje mahali ambapo kila jambo litafanyikia.
  3. Wahusika – Taja mtu au watu waliopewa wajibu wa kutekeleza jambo fulani. Hii huwasaidia kujitayarisha ipasavyo.

Mfano wa Ratiba

RATIBA YA MAZISHI YA MZEE MAUTI TAREHE 20/12/1923 KIJIJINI MIZUKANI

SAA

SHUGHULI

07: 00

Marafiki wa Mauti watoa mwili kutoka SlowDeath Hospital

10: 30

Maombi katika kanisa la G.I.Z.A yakiongozwa na Pst. Muna Fiki

11: 15

Mwili kuwasilishwa nyumbani, familia ya Mauti

12: 00

Kupakuliwa kwa chakula na Bi Kamafisi, Bi Mwachafu na wapishi walioteuliwa

1: 10

Kukusanyika kwa umati

2: 00

Maombi ya kuanzisha shughuli za mazishi

2: 30

Shuhuda zikiongozwa na Mzee Siachwinyuma

3: 00

Ushuhuda wa serikali na Chifu Mtesi

3: 40

Kuteremshwa kwa mwili kaburini na vijana walioteuliwa

4: 00

Shukrani za Mwisho, na Mwenyekiti wa Chama cha Kufa Tukusaidie

6: 00

Kugawana mali ya marehemu, na wazee wa kijiji

Resipe

InshaZa Kiuamilifu • Resipe

Haya ni maandishi yanayotoa maagizo/maelekezo ya kuandaa chakula fulani.

Sehemu muhimu za resipe ni:

  1. Kichwa– Jina la mlo unaoandaa, Idadi ya watu wanaopikiwa
  2. Orodha ya viungo unavyohitaji– majina ya viungo, Idadi au kiasi kinachohitajika
  3. Maagizo/namna ya kupika
  4. Eleza kwa utaratibu kila hatua
  5. Taja wakati utakaotumika katika kila hatua.
  6. Hakikisha kila aina ya viungo ulivyotaja, inajitokeza katika maelezo ya kupika.
  7. Tamati
  8. Baada ya chakula kuiva, eleza kinaweza kupakuliwa na chakula kipi kinginecho k.v ugali na kitoweo cha kuku

Mfano

  1. Andika resipe ya kuandaa mchuzi wa kuku kwa watu watano.
  2. Andika resipe ya kuandaa chakula kwa mgonjwa wa moyo

Tahariri

InshaZa Kiuamilifu • Tahariri

Tahariri ni makala ya mhariri (mkuu) wa jarida/gazeti fulani. Mhariri mkuu hutoa maoni yake kuhusu mojawapo ya maswala ibuka. Sehemu kuu za tahariri ni:

  1. Jina la Gazeti/jarida
  2. Tarehe/nambari ya toleo hilo
  3. Mada ya Tahariri
  4. Ujumbe
  5. Jina la mwaandishi

Wasifu

InshaZa Kiuamilifu • Wasifu

Wasifu ni insha inayosimulia maisha ya mtu fulani tangu kuzaliwa kwake, elimu yake, kazi, ujuzi wake n.k. Anayeandika wasifu ni tofauti na anayezungumziwa katika wasifu huo.

Kuna aina tatu za wasifu:

  • Wasifu wa Kawaida
  • Tawasifu
  • Wasifu-Kazi

Wasifu

Wasifu wa kawaida ni masimulizi ya maisha ya mtu fulani yanayosimuliwa na mtu mwengine. Kwa mfano, Wasifu Wa Siti Binti Saad ulioandikwa na Mwalimu Shaaban Robert.
Katika insha, mwanafunzi anawezaambiwa aandike wasifu wa:

  • mtu mashuhuri- anayejulikana kama vile Nelson Mandela, Julius Nyerere au Mzee Jomo Kenyatta n.k
  • mtu yeyote anayemjua – kama vile mzazi, rafiki, somo(kielelezo), mwalimu wake n.k
  • mtu wa kubuni – mwanafunzi anaweza kubuni mtu na asimulie maisha yake

Tawasifu

Katika tawasifu, mwandishi huwa anasimulia maisha yake mwenyewe. Hivyo basi, tawasifu huandikwa na kusimuliwa katika nafsi ya kwanza.
Katika insha, mwanafunzi anaweza ulizwa asimulie:

  • maisha yake binafsi
  • maisha yake, miaka kadhaa ijayo
  • maisha ya mtu fulani kama yake binafsi k.m ajifanye kuwa Rais wa Tanzania, halafu asimulie maisha yake tangu kuzaliwa hadi alipo. k.m ‘Umekuwa Rais wa nchi yako kwa muda wa miaka mitano, andika tawasifu kuhusu maisha yako itakayowasaidia wananchi wako kukuelewa vyema zaidi
  • maisha ya mhusika wa kubuni, kama yake binafsi

Kwa mfano, katika riwaya ya Siku Njema, mhusika Kongowea Mswahili anaandika tawasifu akisimulia maisha yake tangu kuzaliwa, maisha ya nyumbani, elimu yake, kazi alizozifanya, maono yake n.k

Wasifu-Kazi

Wasifu-kazi (Resume/Curriculum Vitae) ni stakabadhi inayotumiwa kuorodhesha mambo muhimu katika maisha ya mtu kama vile elimu, kazi, ujuzi n.k inayotumiwa sanasana katika kuomba kazi. Kinyume na wasifu na tawasifu ambazo hutumia lugha natharia (ya masimulizi), wasifu-kazi hutumia muundo fulani wa orodha na/au jedwali kuwasilisha mambo muhimu tu. Isitoshe, wasifu kazi huwa fupi – aghalabu ukrasa mmoja.

Tunapoorodhesha mambo fulani katika wasifu, tunaanza na yale ya hivi karibuni hadi yale ya kitambo. Kwa mfano, anza na shule uliyosomea mwisho, iliyokuwa imetangulia hiyo n.k hadi shule uliyoenda kwanza.

Muundo wa Wasifu-Kazi

Katika wasifu-kazi unahitajika kuonyesha:

  1. Jina lako
  2. Namna ya mawasiliano (simu, anwani, barua pepe)
  3. Elimu
    • orodhesha shule zote ulizozisomea kutoka shule uliyosomea mwisho hadi shule ile uliyoihudhuria kwanza.
    • katika kila shule, onyesha miaka uliyohudhuria k.m 1996-2000
    • onyesha shahada (degrees) na diploma ulizozipata
  4. Kazi
    • orodhesha kazi zote ulizozifanya kutoka kazi ya hivi karibuni hadi kazi ulizozifanya mwanzoni
    • onyesha cheo ulichokuwa nacho katika kazi hiyo na majukumu yake
    • onyesha kampuni au mahali ulipofanya kazi hiyo
    • onyesha miaka ambayo ulikuwa katika kazi hiyo
    • taja ujuzi au taaluma uliyoipata katika kazi hiyo
  5. Ujuzi / Taaluma – taja ujuzi maalumu ulionao, taaluma au talanta zozote zinazokufanya
  6. Mapato/Mafanikio/Tuzo – taja mafanikio yoyote au tuzo zozote ulizozipata katika maisha
  7. Mapendeleo – Nini kinakupendeza katika maisha? unapenda kutumiaje muda wako wa likizo usiokuwa wa kazi
  8. Maono ya Kazi – una maono gani katika kufanya kazi? ungependa kufanya nini?

Isimu Jamii• Lugha • Isimu JamiiIsimu Jamii (social

Isimu Jamii

Lugha • Isimu Jamii

Isimu Jamii (social linguistcs) – ni tawi la isimu (elimu ya lugha) linalochunguza namna lugha inavyotumika katika jamii na uhusiano baina yake. Tawi hili huzingatia matumizi ya lugha katika mazingira tofauti; aina mbali mbali za lugha na mazingira yake; uhusiano kati ya lugha na utamaduni wa jamii inayoitumia.

Istilahi za Isimu Jamii

  1. Isimu (linguistics) – ni mtalaa ambao huchunguza, huchanganua na pia kuchambua na kufafanua lugha kama mfumo wa mawasiliano baina ya wanadamu.
  2. Lugha – ni chombo cha mawasiliano baina ya watu. Lugha huzingatia mpangilio maalum wa sauti, maneno na sentensi.
  3. Sajili – ni mukhtadha/rejista mbalimbali au mitindo maalum ya lugha katika mazingira/hali mbalimbali. Mifano ya sajili ni kama vile lugha ya hospitalini, shuleni, sajili ya dini, biashara, kisiasa, michezo,
  4. Fonolojia – ni tawi la sayansi ya isimu linaloshughulikia uchunguzi wa mfumo wa sauti katika lugha fulani, kwa mfano ugawanyaji wa irabu na konsonanti. Fonolojia hutumika kuunda alfabeti katika lugha fulani. Aghalabu kila lugha hutumia mfumo fulani wa sauti mahususi katika lugha hiyo pekee.
  5. Fonetiki – huchunguza sauti zinazotamkwa na binadamu bila kuzingatia lugha yoyote.
  6. Mofolojia – (au sarufi maumbo) ni tawi la isimu linalochunguza maneno ya lugha fulani, aina za maneno katika lugha, hasa upangaji wa mofimu mbalimbali zitumikazo kwa ajili ya kuunda maneno hayo. Kwa mfano, lugha ya Kiswahili hutumia mbinu kadhaa kuunda maneno kulingana na mpangilio wa mofimu. Kwa mfano, neno ‘lima’ linaweza kutumika kuunda maneno mengine katika Kiswahili k.m mkulima, kilimo, nimelima, limika n.k Katika kubadilisha mofimu hizi, tunaweza kubadilisha neno moja kutoka aina moja(kitenzi) hadi nyingine (nomino) n.k
  7. Sintaksi – (au sarufi miundo) ni tawi la isimu au taaluma ya sarufi inayoshughulikia jinsi vikundi vya maneno na sentensi mbalimbali zinajengwa katika lugha. Sintaksia huangazia kanuni au sheria za lugha. Kila lugha huwa na sheria zake za kuambatanisha maneno kama vile jinsi ya kufuatanisha vitenzi, nomino na vielezi. Kwa mfano: Mtoto yako shiba ni sentensi isiyokuwa na sintaksi. Sentensi sawa ingekuwa: Mtoto wako ameshiba.
  8. Semantiki – ni tawi la isimu linalochunguza maana halisia (mantiki) ya maneno, kifungu au sentensi katika lugha. Sentensi isiyokuwa na mantiki ni sentensi inayotoa maana ambayo haiwezekani katika uhalisia. Sentensi inaweza kuwa sawa kisintaksia lakini iwe na makosa ya kimantiki. Kwa mfano: Kiatu cha mbwa kimefutwa kazi kwa sababu kumi ni kubwa kama hewa.

Sajili Katika Isimu Jamii

LughaIsimu Jamii • Sajili

Sajili – ni mukhtadha/rejista mbalimbali au mitindo maalum ya lugha katika mazingira/hali mbalimbali.

Kuna sajili anuwai za matumizi ya lugha katika jamii. Hapa tutazingatia mifano michache ya sajili mbali mbali.Kila sajili huwa na sifa mbalimbali zinazoitofautisha sajili hiyo na nyinginezo. Ili kubaini sifa za lugha katika sajili fulani, ni muhimu kuzingatia baadhi ya maswali yafuatayo:

  • ni mazungumzo baina ya nani na nani?
  • kuna uhusiano gani baina ya wanaozungumza?
  • yanapatikana wapi?
  • yanatumika katika hali gani?
  • yana umuhimu ama lengo gani
  • ni istilahi zipi istilahi (maneno maalum) zinazopatikana katika mazingira hayo?
  • umaizi wa lugha baina ya wazungumzaji ni wa kiwango gani?
  • ni mtindo gani wa lugha unaotumika?

Sajili ya Ajali

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Ajali

Hii ni lugha inayotumiwa katika ambalo ajali imetokea. Wahusika wanaweza kuwa majeruhi, polisi, walioshuhudia au wananchi wengine n.k

Sifa za lugha inayopatikana katika sajili hii

  1. Msamiati wa kipekee unaohusiana na ajali kama vile majeruhi, hudumanya kwanza, damu, mkasa.
  2. Hutumia lugha ya kudadisi dadisi ili kubaini chanzo cha ajali.
  3. Huwa na masimulizi – walio na habari kuhusu kisa hicho hueleza waliyoshuhudia
  4. Kutokana na hali ya msukosuko, lugha hii haina utaratibu – watu huwa katika hali ya hofu, kwa juhudi za kuwaokoa majeruhi.

Mfano wa Sajili ya Ajali

Mwanakijiji 1:

Nimesikia twa! Kisha kishindo kikubwa sana (akihema hema) Nikaambia kuna mlipuko tukimbie.

Mwanakijiji 2:

Lilio la muhimu ni kuyaokoa maisha ya majeruhi kwa kuwapa huduma ya kwanza.

Mwanakijiji 1:

Tuondoeni miili ya waliofariki kwanza.

Mwanakijiji 2:

hatuwezi kuishika miili iliyobanwa katika gari hadi polisi wafike. Na ndio hao wanaokuja!

Mwanakijiji 1:

(akikimbia) Ndio hao! Acheni kuiba mafuta! Polisi wanakuja!

Polisi:

Wakitawanya wananchi walioliparamia gari kuiba bidhaa mbali mbali.Liinueni hili gari! Wapi dereva?

Dereva:

(ambaye amelala akihema kwa maumivu, damu ikichuruzika miguuni na mikononi) Nilisitishwa na ng’ombe waliokuwa wakivuka barabara. Nilijsribu kukwepa lakini usukani ukanishinda gari likapoteza mwelekeo…

Abiria:

Alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana. Tukampigia kelele apunguze mwendo lakini hakutusikia. Matunda yake…

Mwanakijiji 2:

Niliona gari likibingiria mara kadhaa mpaka likaingia humu mtaroni, ndiyo tukakimbia kuwaokoa.

Polisi:

Nyamazeni! Achieni polisi kazi iliyobaki. Ikiwa kuna yeyote anayejuana na waathiriwa aandamane nasi.

Sajili ya Biashara

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Biashara

Lugha ya biashara huzungumzwa na wauzaji na wanunuzi katika sehemu za kibiashara. Inapaswa ikumbukwe kwamba lugha hii inaweza kubadilika kidogo kulingana na mazingira. Kwa mfano, katika mikutano ya kibiashara, lugha rasmi hutumiwa ilihali katika soko, lugha ya mitaani inaweza kutumika.

Sifa za Lugha ya Biashara

  1. Hutumia msamiati wa kibiashara kama vile:
    • Fedha
    • Faida
    • Hasara
    • Bei
    • Bidhaa
  2. Hutumia misimu ili kuwavutia wanunuzi
  3. Ni lugha yenye malumbano hasa watu wanapojadiliana kuhusu bei
  4. Ni lugha legevu – haizingatii kanuni za lugha.
  5. Huchanganya ndimi kwa kuingiza maneno ya lugha za kigeni
  6. Ni yenye heshima na unyenyekevu kwa wanunuaji
  7. Msamiati katika lugha ya Kibiashara

Mfano wa Sajili ya Biashara

Mtu X:

Tatu kwa mia! Tatu kwa mia! Leo ni bei ya hasara!

Mtu Y:

Unauza hii briefcase kwa pesa ngapi?

Mtu X:

Hiyo ni seventy bob mtu wangu

Mtu Y:

Huwezi kunipunguzia. Niuzie hamsini hivi.

Mtu X:

Haiwezekani mtu wangu. NItapata hasara nikiuza hivyo. Ongeza mkwaja, mama.

Mtu Y:

Basi hamsini na tano.

Mtu X:

Tafadhali ongeza kitu kidogo. Unataka nikule hasara leo? Fikisha sitini na tano.

Mtu Y:

Basi sitanunua hii. Sina pesa hizo zote. Unajua uchumi ni mbaya siku hizi.

Mtu X:

Tafadhali mtu wangu. Huu mkoba ni mzuri sana. Umetoka Germany. Angalia. Unaweka pesa hapa, kitambulisho hapa halafu unafunga hivi. Hauwezi kupoteza chochote ukiwa na mkoba huu. Angalia wewe mwenyewe. Hakuna mahali pengine utaweza kununua mkoba huu kwa bei ghali kama hii.

Mtu Y:

Nimekwambia sina hizo pesa. Nitanunua baadaye ukipunguza bei.

Mtu X:

Lete sixty bob. Lakini utakuwa umeniumiza. Nakufanyia hivyo kwa kuwa wewe ni customer poa.

Mtu Y:

Sawa basi nitanunua. Shika sixty bob.

Mtu X:

Asante Customer. Mungu akubariki. (akimfungia) Hey! Tatu kwa mia. Bei ya hasara! Tatu kwa mia!

Sajili ya Bungeni

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Bungeni

Hii ni lugha inayozungumzwa wakati wa kikao cha bunge. Sajili hii ni tofauti na na sajili ya siasa, ambayo huhusisha wanasiasa wakipiga kampeni.

Sifa za Lugha ya Bungeni

  1. Ni lugha yenye ushawishi – wabunge hutumia vishawishi ili kuwahimiza wenzao waunge ama kupinga msalaba
  2. Ni lugha ya mjadala yenye waungao na wapingao.
  3. Ni lugha yenye heshima na nidhamu. Maneno ya heshima kama mheshimiwa, tafadhali na samahani hutumika sana.
  4. Hutumia maneno maalum yanayopatikana katika mazingira ya bunge kama vile kikao, mswaada, kuunga mkono, kujadili, kupitisha, n.k.
  5. Lugha ya bungeni ni rasmi na sanifu.
  6. Hulenga maswala mbalimbali ya kisiasa na maendeleo katika taifa.
  7. Huwa na maelezo kamilifu
  8. Ni lugha yenye maswali na majibu miongoni mwa wabunge.

Mfano wa sajili ya Bungeni

Spika:

Waheshimiwa, muda unayoyoma. Nawaomba mfanye mazungumzo yenu sauti ya chini tumsikize huyu. Endelea mheshimiwa.

Mbunge 1:

Asante Bwana spika. Hii siyo mara ya kwanza ya kuuwasilisha mswaada huu hapa. Kila mbunge anayethamini raia wa taifa hili ni lazima auunge mkono mswada huu. Katika kikao kilichotangulia, mliupinga mkidai kwamba hauna heshima kwa rais. Leo tumefanya ukarabati wote mliotaka. Hamna budi kuuunga mkono. Bwana spika….

Spika:

Muda wako umekwisha tafadhali keti. Wabunge wataamua hatima ya mswada huu ikiwa utapitishwa kama sheria. Lakini kumbukeni uamuzi wa mwisho ni wa rais.

Sajili ya Hospitalini

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Hospitalini

Hii ni lugha ambayo huzungumzwa katika hospitali baina ya madaktari, wagonjwa, wauguzi n.k

Sifa za Lugha ya Hospitalini

  1. Hutumia msamiati wa hospitalini kama vile
    • dawa
    • magonjwa
    • Daktari
    • Wadi
    • Mgonjwa
    • Dawa
    • Kipimo
  2. Ni lugha yenye upole na heshima
  3. Huwa na maswali mengi hasa daktari anapotaka kutambua kiini cha ugonjwa unaomhadhiri mgonjwa wake
  4. Ni lugha yenye hofu na huzuni

Mfano wa Sajili ya Hospitalini

Daktari:

Ulianza kuumwa hivi lini?

Mgonjwa:

Kichwa kilianza kuniuma jana jioni baada ya chajio. Nilipoamka asubuhi nikatambua kwamba hata tumbo lilikuwa likiuma pia.

Daktari:

Ulipoanza kuumwa na mwili mzima, ulichukua hatua gani? Hukunywa dawa yoyote?

Mgonjwa:

Nilichukua tembe zilizokuwa zimepatiwa kakangu miaka mitano iliyopita alipokuwa akiumwa na malaria.

Daktari:

Kila ugonjwa huitaji matibabu mbalimbali. Tembe za malaria haziwezi kutumika kutibu maumivu ya kichwa na tumbo. Pia ni hatari kutumia dawa ambazo zimepitwa na wakati. Zinaweza kukuletea madhara zaidi.

Mgonjwa:

(akikohoa) Sijui kama una tembe za kifua pia. Hii baridi inaniletea homa mbaya.

Daktari:

Hatuwezi kukupatia dawa kabla ya kutambua ugonjwa ulio nao. Itabidi tupime joto lako, damu na pia mate yako ili kupata tatizo linalokusumbua. Kisha tutakupatia dawa. Je, una umri wa miaka mingapi?

Mgonjwa:

Nikichukua hizo dawa nitapona?

Daktari:

Matokeo hubadilika kutoka kwa mgonjwa mmoja hadi mwengine. Inaweza kuchukua muda. Huenda ukalazwa kwenye wadi kwa siku mbili tatu hivi. Umri wako, mama?

Sajili ya Kidini

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Kidini

Katika sajili ya kidini tunaangazia lugha inayozungumzwa na waumini/washiriki wa imani fulani wakati wa ibada, sala, katika nyumba takatifu au mahali popote pale ambapo wanazungumzia mambo yanayorejelea imani au Mwenyezi Mungu.

Sifa za Lugha ya Kidini

  1. Hutumia msamiati wa kidini kama vile
    • Bibilia
    • maombi
    • mbinguni
    • jehanamu
    • Madhabahu
    • Paradiso
    • Mbinguni
    • Mwenyezi Mungu
    • Mwokozi
  2. Ni lugha inayonukuu sana hasa wazungumzaji wanaporejelea Kitabu kitakatifu
  3. Lugha yenye heshima, upole na unyenyekevu
  4. Lugha sanifu
  5. Ni lugha iliyojaa ahadi nyingi kwa wanaoandamana na mafunzo ya kidini na vitisho kwa wanaoenda kinyume na mafundisho
  6. Huwa imejaa matumaini
  7. Ni lugha yenye kutoa maneno ya sifa, kumtukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu

Mfano wa Sajili ya Kidini

Boriti:

Bwana asifiwe Bi…

Bi Rangile:

Amina, mchungaji. Watoto wanaendeleaje?

Boriti:

Karita hana neno. Mwenyezi Mungu ametunyeshea rehema na neema zake. Je, wajukuu wako wa hali gani?

Bi Rangile:

Wanaendelea vizuri isipokuwa hawataendelea na masomo. Sijui nilimfanyia Mungu dhambi gani.

Boriti:

Nasikitika sana kusikia hivyo. Mungu atawalinda mayatima hao. Yeye ndiye baba wa mayatima. Mungu ni mwenye huruma.

Bi Rangile:

Sijui hayo, mchungaji. Hata sijui maana ya kuishi hapa duniani. Kila siku ni matatizo.

Boriti:

Usife moyo. Mungu anasema katika kitabu cha Yohana 14:18, “Sitawaacha nyinyi kama mayatima…” Kwa hivyo, ukiwa na imani, Mungu atakuonekania.

Bi Rangile:

Basi niombee mchungaji ili Saumu na Neema wapate karo ya kurudi shuleni.

Boriti:

Funga macho tusali. Ewe Rabuka uliyejaa neema na baraka tele. Tunakushukuru na kulitukuza Jina lako takatifu kwa baraka zako za ajabu. Tunajua kwamba wewe ndiye Mungu uliyewatoa wana wa Israeli kutoka Misri. Sisi wenye dhambi tunakuja mbele yako tukiomba ukafanya miujiza katika nyumba hii ya Bi Rangile……

Wote:

Amina.

Sajili ya Kisayansi

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Kisayansi

Sifa za Lugha katika sajili hii

  1. Hutumia msamiati wa kipekee unaoambatana na taaluma inayorejelewa.
  2. Huwa na maelezo kwa ukamilifu.
  3. Huwa na mpangilio maalum na maendelezo ya hoja na ujumbe.
  4. Huchanganya ndimi na kutumia maneno ya kisayansi au lugha mbalimbali.
  5. Hutumia lugha sanifu.
  6. Ni lugha yenye udadisi mwingi (wakati wa kufanya utafiti)
  1. Kwa sababu zisizoweza kuepukika, kikundi chetu hakitamaliza utafiti ulioratibiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi ujao. Hii ni kwa sababu ya changamoto kadhaa ambazo tumekutana nazo. Kwanza, viluwiluwi, ambao ndio tunaotafiti wamekuwa haba sana wakati huu wa ukame. Pili, kutokana na kufungwa kwa maabara ya kisayansi katika taasisi hii, ni muhali kufanya majaribio yoyote ya kazi yetu. Tatu, kumekuwa na pingamizi kubwa kutoka kwa baadhi ya wanakijiji kwamba kukusanya viluwiluwi kunawatia hofu. Aidha, tume yetu imepungukiwa na fedha baada ya serikali kusitisha kudhamini utafiti huu.
  2. Baada ya kujadiliana kwa vikao tatu mfululizo, tume yetu inapendekeza haya: Muda wa kufanya utafiti uongezewe kwa kipindi cha miezi sita; serikali kupitia kwa taasisi hii ifadhili wachunguzi. Wananchi wahamasishwe kuhusu umuhimu wa kuwafanyia viwavi utafiti na maabara ya utafiti ikaraatiwe haraka iwezekanayo.

Sajili ya Mahakamani

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Mahakamani

Hii ni lugha inayozungumzwa na wanasheria, mahakimu, mawakili, washitakiwa na mashahidi katika mahakama.

Sifa za Lugha ya Mahakamani

  1. Hutumia msamiati wa kipekee unaorejelea sheria kama vile
    • katiba
    • sheria
    • mashtaka
    • Hakimu
    • Ushahidi
    • Wakili
    • Jela
    • Mshitakiwa
    • Kiongozi wa mashtakiwa
  2. Huwa na maelezo marefu na ya kina ili kutafuta ushahidi wowote uliopo
  3. Ni lugha yenye kunukuu sana hasa vipengele katika vitabu vya sheria kama vile katiba
  4. Ni lugha rasmi na sanifu
  5. Ni lugha iliyojaa maswali na majibizano
  6. Ni lugha yenye heshima

Mfano wa Sajili ya Mahakamani

Kiongozi:

Musa Kasorogani, mwanaye Bi Safina na Mzee Mpotevu Kasorogani; umeshtakiwa kwa kosa la jaribio la mauaji mnamo tarehe 23/08 mwaka huu. Unaweza kukubali mashitaka, kukana au kunyamaza. Je, unakubali mashitaka.

Musa:

Naomba kukanusha mashtaka hayo, bwana mkubwa.

Kiongozi:

Je, kuna shahidi yeyote katika kesi hii?

Katili:

Hapa mkubwa. Siku hiyo ya tarehe 23/08, Musa alipatikana akiwa akijinyonga usiku wa maneno. Kijiji chote kilikusanyika hapo kwenye boma ya Kasorogani. Nilipoleta polisi, wakamkamata na kumpeleka hospitalini atibiwe kwanza. Ndiposa ameletwa hapa siku ya leo.

Kiongozi:

Je, mshitakiwa una tetesi lolote. Ama pia unaweza kuleta wakili wako azungumze kwa niaba yako.

Kisaka:

Bwana mkubwa, mimi ndiye wakili na shahidi wa Musa. Musa hakuua mtu. Alikuwa akijinyonga kutokana na mkasa uliomfika tarehe hiyo ya Agosti 23 baada ya bibi harusi wake kubadilika. Mimi na mamake, Bi Safina Kasorogani tulijaribu kumtuliza jioni hiyo. Asubuhi nilipoamka siku iliyofuatia, nikapata habari kwamba alikuwa amepelekwa hospitalini. Je, alipojaribu kujiua, alimwua mtu yeyote?

Kiongozi:

Kulingana na katiba ya nchi hii, kifungu cha 12.ab, kuua ni kutoa uhai wa binadamu yeyote. Haijalishi ikiwa ni yeye mwenyewe au ikiwa ni rafiki yake. Hivyo basi jaribio la kujiua ni hatia kulingana na kanuni za nchi hii. Una jingine la kuulizia?

Kisaka:

Je, sheria yetu inaruhusu mtu kuadhibiwa kwa kosa ambalo hakufanya?

Kiongozi:

La hasha.

Kisaka:

Basi tutakuwa tumekiuka kanuni za nchi yetu iwapo tutamhukumu Musa kwa kujiua ilhali hakujiua bado. Tunawezaje kutambua kama angekufa?

Katili:

Inafaa ahukumiwe kinyonga au kifungo cha maisha gerezani. Hata alivunja simu yangu…

Kiongozi:

Order! Lazima kutii mpangilio wa mahakama. Katili hauruhusiwi kuongea bila ruhusa ya hakimu au kiongozi wa mashitaka. Polisi, mpelekeni nje.

Sajili ya Matanga

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Matanga

Ni lugha inayotumiwa katika shughuli za mazishi au nyumbani kwa marehemu.

Sifa za Lugha ya Matanga/Mazishi

  1. Hutumia msamiati wa maneno ya huzuni kama vile waombolezaji, makiwa, kifo, mauti, pole n.k.
  2. Hutumia lugha ya kuliwaza/kufariji na kupa matumaini hasa kwa waombolezaji.
  3. Ni lugha yenye unyenyekevu isiyotumia maneno yanayokera.
  4. Hudhihirisha unyonge wa mwanadamu, kama asiye na mamlaka juu ya uhai wake.
  5. Huwa na mbinu rejeshi kurejelea maisha ya marehemu alipokuwa hai.
  6. Kwa mara nyingi hutumia maneno ya kusifu marehemu kutokana na aliyotenda.
  7. Wakati mwingine huwa ni lugha inayodhihiri hali ya kukata tamaa.

Mfano wa Sajili ya Matangani

“Waombolezaji wenzangu, kama mnavyojua tumekusanyika hapa kwa ajili ya kumsindikiza rafiki yetu amabye amelala hapa. Ikiwa kuna mtu alifikwa zaidi na msiba huu ni mimi. Marehemu alikuwa rafiki wangu wa dhati tuliyeshirikiana naye sana. Nilimjua marehemu tukifanya kazi katika soko la Mauzoduni na tangu siku hiyo tumeishi kama ndugu; kuomba radhi ukikosewa; kusaidiana, na kadhalika.

Habari za kifo chake zilinipiga kwa mughdha. Sikuamini kwamba amekufa; kwamba sitamwona tena aushini mwangu. Ninasikitika sana lakini kwa kuwa Mungu hakosi, ninaamini kwamba alimpenda zaidi ya tulivyompenda. Ombi langu kwa Mungu ni moja, kwamba amweke rafiki yangu mahali pema peponi; au popote alipojitafutia siku zake za uhai; nami nitakapokufa anipeleke papo hapo tuendelee kuwa marafiki. Mwenzangu lala. Lala salama tutaonana siku moja”

Sajili ya Michezoni

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Michezoni

Lugha ya michezoni hutumiwa wakati wa mashindano ya michezo kama vile kandanda, ukimbiaji n.k Hii inaweza kuwa lugha ya watangazaji/wasimulizi wa mchezo, watazamaji, mashabiki au wachezaji.

Sifa za Lugha ya Michezoni

  1. Hutumia msamiati wa kipekee unaohusu michezo kama vile mpira, goli, mchezaji
  2. Huchanganya ndimi na kuingiza maneno ya lugha nyingine kama vile Kiingereza. mfano ‘goal!!!’
  3. Ni lugha ambayo hutumia vihisishi na mshangao kwa wingi
  4. Sentensi nyingi katika lugha hii huachwa bila kukamilika hasa hali inapobadilika uwanjani
  5. Husimuliwa kwa haraka haraka ili kuambatana na kasi ya mchezo
  6. Ni lugha yenye sifa na na chuku kwa mfano msimulizi anaposimulia sifa za mchezaji fulani
  7. Hutumia misimu kama vile ‘wametoka sare’
  8. Hutumia kwa ya kulinganisha ili kuelezea matokeo ya mechi k.m ‘walitoka mbili kwa nunge’
  9. Ni lugha yenye kukariri (kurudia rudia) hasa mchezaji anapoumiliki mpira kwa muda mrefu au mwanariadha fulani anapoelekea kushinda katika mbio.
  10. Huwa na sentensi fupi fupi

Mfano wa Sajili ya Michezoni

Nakwambia ndugu msikilizaji hapa mambo yamechacha kwelikweli. Hawa wachezaji wa Manyuu hawacheki na watu leo. Wameamua kuishambulia timu ya Cheusi bila huruma. Kumbuka kwamba hii ni mara yao ya… Lo! Anauchukua mpira pale, mchezaji nambari tisa… Matiksta. Matiksta, Matiksta na mpira. Anaucharazacharaza pale. Anamwangalia mwenzake. Anaupiga mpira kwa kichwa pale! Lo! Mwenzake anaukosa. Akiushika mpira pale ni mchezaji wa timu ya Cheusi, Romana. Romana, Romana anaelekeza mpira kwenye lango la Manyuu. Anaupiga mpira kwa nguvu! Lo! Hatari sana. Hatari sana katika lango la Manyuu. Hatari! hatari! Goooooooooo ooooh! Wameukosa! Goal keeper ameudaka mpira huo. Pole sana wachezaji wa … Mlinda lango anaupiga mpira huo kwa hasira. Juu kabisa. Anauchukua pale nambari saba, Saruta. Huyu ni mchezaji machahari sana. Mwaka uliopita, alipewa tuzo la mchezaji bora wa mwaka. Ananyang’anywa na mchezaji mwingine hapa. Wanakabiliana kidogo. Huyu mchezaji anaupiga mpira kwa mguu wa kushoto. Lo! Mpira umekuwa mwingi na ukatoka nje.

Sajili ya Mtaani

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Mtaani

Lugha ya mitaani ni lugha inayozungumzwa na vijana mtaani.

Sifa za Lugha ya Mtaani

  1. Ni lugha legevu isiyozingatia kanuni za kisarufi
  2. Huchanganya ndimi
  3. Hutumia misimu kwa wingi
  4. Hukosa mada maalum

Mfano wa Sajili ya Mtaani

Chali:

Hey, niaje msupaa?

Katosha:

Poa. So, mathee yako alikushow naweza kuja?

Chali:

Ha! Masa hana noma. Si unajua nita…

Katosha:

Chali! Unataka aniletee problem?

Chali:

Mimi ni boy wa maplans. Ngoja nifikirie venye tutamshow

Katosha:

Na by the way, kwani umejipaka mafuta ya manzi. Ama ulikuwa na msichana mgani?

Chali:

Oh! Niliscoop mafuta ya Anita. Si unajua nataka kunukia hmmmm…

Katosha:

Ok. So, umefikiria tumshow nini masa yako? Ama nikona idea poa.

Chali:

Nishow hiyo plot, na by the way, nataka unisaidie kuhusu ile deal yangu na Kaunda. Ile ya siz yangu.

Katosha:

Kwanza tutaplan na huyo siz yako, niwe ndiye nimekuja kuvisit. Mamako atakubali

Chali:

Wow! Idea poa. Utakuwa umekuja kufanya homework. Halafu masa akiishia kwa bed. Homework tutaitupa mbali.

Katosha:

So, utamshow Anita nakuja tufanye homework…

Sajili ya Nyumbani

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Nyumbani

Hii ni lugha inayotumiwa na watu katika familia. Wanaohusika sana katika mazungumzo ya nyumbani ni mama, baba, watoto, majirani na watu wa ukoo. Maswala yanayorejelewa sana ni yale yanayoiathiri jamii/boma hilo.

Sifa za Sajili ya Nyumbani

Sifa za sajili ya nyumbani hubadilika kulingana na mada inayorejelewa, wanaozungumza na hali katika boma.

Mfano wa sajili ya nyumbani

Baba:

Mama Kadara! Huyo mtoto wako amekuja?

Mama:

Kadara ni mtoto wetu; mimi na wewe.

Baba:

Hapana! Mimi sizai malaya. Huyo ni wako. Hata Bahati ni wako! Hakika wote sita ni wako…

Mama:

Mume wangu unanifanya nikasirike bure tu. Mbona umeanza mafarakano tena.

Baba:

Mafarakano! Mafarakano! Ni mimi niliyekwambia uzae wasichana sita…

Mama:

Lakini sikuzaa pekee. Tulizaa na wewe, mume wangu….

Baba:

Hapana! Uliniona na mimba? Uliniona na maumivu ya uzazi? Umeniona nikinyonyesha mtoto? Mwanamke kuwa na adabu. Nitakurudisha kwa wazazi wakufunze heshima. Na nitaoa sioni tukikaa pamoja.

Mama:

(baada ya kimya) Niambie ulichotaka kuniambia kuhusu Kadara (akijipangusa machozi kwa kitambaa) unajua mume wangu, nakuheshimu. Yangalikuwa mapenzi yangu tungepata wavulana pia. Lakini haya ni mapenzi ya Mungu.

Baba:

Kadara akija umpe kuku apeleke vileoni kwa Mzee Magoti. Nina deni lake kubwa baada ya kunywa tembo siku kadhaa bila kulipa. (akicheka) Hakika hata anastahili mbuzi.

Mama:

Hatuwezi kulipia pombe kwa mbuzi wala kuku. Kuku waliobaki hapa ni wangu na wa watoto wangu. Kuku wako uliwauza.

Baba:

Kelele za chura hazimkatazi ng’ombe kunywa maji. Endelea kupayuka kama wanawake wengine wa kijijini. Nikirudi nikute chakula na maji moto tayari.

Mama:

(akinuna) Haya nimesikia.

Sajili ya Shuleni

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Shuleni

Hii ni rejista ya lugha inayopatikana katika mazingira ya shule. Wahusika wake huwa walimu, wazazi na wanafunzi.

Sifa za Sajili ya Shuleni

  1. Matumizi ya istilahi (maneno maalum) yanayopatikana katika mazingira ya shule kama vile darasa, mitihani, vitabu, elimu, muhula, masomo
  2. Lugha yenye heshima kutokana na utofauti baina ya mwanafunzi na mwalimu, mzazi na mwalimu;
  3. Takriri – mbinu ya kurudiarudia maneno. Katika darasa mwalimu hurudia rudia maneno ili kusisitiza anachofunza
  4. Ni lugha yenye maswali mengi na majibu. Mwalimu huuliza maswali wakati wa mafunzo. Wanafunzi pia huuliza maswali ili kujua/kupata ufafanuzi.
  5. Hutumia lugha ya kukosoana na kurekebishana.

a) Mfano wa Mazungumzo katika Sajili ya Shuleni

Mwalimu:

Mzee Kundu, ningetaka tuzungumze kwa muda kuhusu hali ya mwanao, Machome Kundu.

Mzee:

Machome? Ana nini mwanangu.Kuna nafasi imepatikana ya…

Mwalimu:

Mwanako amebadilika sana kitabia. Alikuwa akifanya vizuri sana katika masomo

Mzee:

Kweli kabisa. Mimi ni mlezi mwema sizai watoto mbu mbu mbu darasani.

Mwalimu:

Ndivyo. Lakini sasa naona ameanza kubadilika. Ameanza kulegea katika mitihani na kuzembea kazini.

Mzee:

Unamaanisha nini? (akiinuka) Inaonekana siku hizi hamjui kuwapa adabu watoto. Ni lazima mtoto wangu amepotoshwa na wengine, katika vikundi vibaya!

Mwalimu:

Hakika, mwanako ndiye anayepotosha wanafunzi wengine. Yeye ni kiongozi wa makundi haramu shuleni, yanayovuruga masomo, kuuza dawa za kulevya na mambo kama haya. Hii ndiyo sababu nimekuita tujadiliane. Ni lazima mienendo hii imechipuka nyumbani.

Mzee:

Ajapo nyumbani, mwanangu huzingatia vitabu pekee hata mamake anaweza kuthibitisha haya. Ikiwa kuna utovu wa nidhamu nina hakika haya yanatoka darasani.

Mwalimu:

Tafadhali keti mzee (akichungulia dirishani) Mtindi! Niitie Machome…

b) Mfano wa Mazungumzo katika Sajili ya Darasani

Mwalimu:

Toeni vitabu vyenu vya Historia mnakili haya. Ni nani atakayetukumbusha tulichosoma wiki jana? Naam Halima!

Halima:

Tulisoma kuhusu Chama cha Mapinduzi

Wanafunzi:

(Wakiinua mikono na kupiga kelele) Mwalimu Mwalimu

Mwalimu:

Inueni mikono nitawaona. Msipige kelele. Halima umenoa. Simama! Mwanafunzi mwengine?

Jadaha:

Tulisoma kuhusu kundi asi la Maji Moto lililopinga wakoloni.

Wanafunzi:

Mwalimu! Mwalimu! Kundi la Maji Maji.

Mwalimu:

Naam mmepata. Lakini nimewaambia msijibu kwa pamoja. Ukitaka kujibu uinue mikono. Jadaha, ni kundi la Maji Maji siyo Maji Moto. Leo tutasoma athari za kundi katika taifa letu la Tanzania na namna lilivyoshindwa nguvu. Lakini kabla hatujaendelea ningependa mniambie, ni matatizo yepi yaliyochochea kuchipuka kwa kundi hilo.

Kirata:

Mwalimu nina swali. Kiongozi wa kundi hilo alikuwa nani?

Mwalimu:

Kirata hukuwa darasani wiki jana. Nione baada ya kipindi hiki. (wanafunzi wakicheka) Nawe wafanyani na kitabu cha Hisabati katika somo la Historia. Kimbia ofisini uniletee kiboko. Ninyi ndio mnaorejesha nyuma darasa langu katika mitihani.

Sajili ya Simu

Isimu JamiiSajili • Sajili ya Simu

Hii ni lugha inayotumiwa katika mazungumzo ya simu.

Sifa za lugha ya simu

  1. Mazungumzo ya simu ni mafupi, hutumia sentensi fupi zenye muundo rahisi.
  2. Hoja hutajwa moja kwa moja bila maneno mengi kwani ili kudhibiti gharama ya simu
  3. Huwa na kukatizana kwa maneno kati ya wazugumzaji.
  4. Huwa ni mazungumzo baina ya watu wawili pekee; anayepiga na anayepokea.
  5. Hutumia istilahi maalum za lugha ya simu kama neno ‘hello’
  6. Huchanganya ndimi (kutumia maneno yasiyo ya lugha nyinginezo) ili kuwasilisha ujumbe kwa upesi.
  7. Ni lugha ya kujibizana.

Mfano wa Sajili ya Simu

Sera:

Hello. Ningependa kuongea na Mika.

Sauti:

Subiri kidogo nimpatie simu.

Sera:

Hello

Mika:

Hello. Sema Sera. Niko kwa mkutano…

Sera:

Pole kwa kukusumbua. Unakumbuka safari yetu ya kesho?

Mika:

Siwezi kusahau. Tunakutana saa ngapi?

Sera:

nampendekeza saa tano machana…

Mika:

Katika Hoteli ya Katata Maa

Sera:

enhe. Hapo kwa heri

Mika:

Haya. Bye!

Tamathali za Usemi• Faishi • Tamathali za UsemiTamathali

Tamathali za Usemi

Faishi • Tamathali za Usemi

Tamathali za Usemi ni matumizi ya maneno kwa namna fulani ili kuifanya lugha iwe ya kuvuitia na kuifanya kazi ya sanaa iwe ya kupendeza. Kuna aina mbili za tamathali za usemi:

  1. Mbinu au Fani za Lugha– Ni uteuzi wa maneno ili kuifanya lugha iwe ya kupendeza na kuvutia. Pia, Mapambo ya Lugha. Fani za Lugha zinaweza kutambulikana moja kwa moja bila kusoma kifungu kizima.
  2. Mbinu za Sanaa– Ni ubunifu wa kisanaa unaojitokeza baada ya kusoma au kusikiliza masimulizi. Angalau unahitaji kusoma sentensi kadhaa au hata hadithi nzima ili kutambua mbinu ya sanaa iliyotumika.

Fani za Lugha

Tanakali za Sauti

Ni mbinu ya kutumia maneno yanayoiga sauti au hali fulani au namna kitendo kilivyofanyika. Milio.

Tashbihi

Hii ni mbinu ya lugha inayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha; ‘kama’, ‘mithili ya’, ‘sawa na’, ‘ja’. Tashbiha. Similes.

Tashihisi

Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai (sifa za kibinadamu). Uhuishaji. Personification.

Takriri

Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. Repetition

Tanakuzi

Tanakuzi ni mbinu ya kusisitiza ujumbe kwa kuambatanisha maneno ya kinyume au yanayokinzana. Ukinzani

Istiara

Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kutumia kiungo ‘ni’ ama ‘kuwa’. Istiari. Sitiari. Imagery

Taswira

Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji.

Taashira

Ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika kumaanisha kitu kingine chenye uhusiano na kile kilichotumiwa. Symbolism

Jazanda

Ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi.

Majazi

Majazi ni pale tabia za wahusika zinapoambatana na majina yao halisi.

Lakabu

Ni mbinu ya mhusika kupewa/kubadikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia/sifa zake.

Chuku

Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe fulani au kusifia kitu. Kutilia Chumvi. Hyperbole

Semi

Ni fungu la maneno linapotumika kutoa maana nyingine, badala ya ile ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha ukali wa maneno au kupamba lugha. Kuna aina mbili za semi:

  • Nahau – huwa na vitenzi
  • Misemo – haina vitenzi

Maswali ya Balagha

Tashititi au maswali ya balagha ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika ambayo hayahitaji jibu. Mubalagha. (Rhetorical questions)

Uzungumzi Nafsiya

Mhusika hujizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.

Ritifaa

Mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa (au asiyekuwepo) kana kwamba yuko pamoja nawe.

Utohozi

Kutohoa ni mbinu ya kuswahilisha maneno ya lugha nyingine, yatamkike kama ya Kiswahili.

Kuchanganya Ndimi

Kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili.

Kuhamisha Ndimi

Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu.

Methali

Methali ni misemo ya hekima yenye maana iliyofumbwa. Mhusika, mwandishi wa fasihi anaweza kutumia methali kupitisha ujumbe.

Mbinu za Sanaa

Kinaya

Kinaya ni mambo katika sanaa kuwa kinyume na matarajio ya hadhira. Irony

Kejeli

Kejeli ni mbinu ya sanaa inayotumia maneno kudharau au kukemea kitendo au mtu fulani.

Taharuki

Taharuki ni mbinu ya kusimulia au kuandika riwaya/hadithi kwa kufanya hadhira na/au wahusika wajawe na hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye; hamu ya kutaka kuendelea kusoma/kusikiliza. Baadhi ya hadithi huishia kwa taharuki na kuilazimisha hadhira yake ijikamilishie au ibaki ikijiuliza maswali. Suspense

Sadfa

Sadfa ni kugongana kwa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vilikuwa vimepangwa, japo havikuwa vimepangiwa. Coincidence

Kisengere Nyuma

Mwandishi ‘hurudi nyuma’ na kuanza kusimulia kisa kilichokuwa kimetendeka kabla ya alichokuwa akisimulia. Aidha, mwandishi hubadilisha wakati wa masimulizi na kuwa wakati wa kisa hicho. Hutumika sana kuonyesha mhusika anapokumbuka kitu, au kutupatia msingi wa jinsi mambo yalivyoanza. Mbinu Rejeshi. Flashback

Kisengere Mbele

Mwandishi anapobadilisha wakati na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni; au kutumia lugha isiyo moja kwa moja kutabiri yatakayojiri. Utabiri. Foreshadow

Njozi au Ndoto

Mwandishi hutumia ndoto kutabiri jambo litakalofanyika au kufumbua jambo lililokuwa limefumbwa.

Upeo wa Juu

Ni sehemu ya hadithi ambayo matukio yanafanyika kulingana na mapenzi ya hadhira au msomaji. Climax

Upeo wa Chini

Ni sehemu ya hadithi ambayo matukio yanafanyika kinyume na mapenzi ya hadhira au msomaji. Aghalabu upeo wa chini hutokea baada ya upeo wa juu. anti-climax

Nyimbo

Nyimbo na/au mashairi yanaweza kutumika katika hadithi kwa madhumuni mbalimbali.

TamthiliaTAMTHILIAVisaweTamthiliyaUtanzu wa FasihiFasihi Andishi  MifanoMstahiki MeyaKifo KisimaniShamba la WanyamaAngaliaAina

Tamthilia

TAMTHILIA

Visawe

Tamthiliya

Utanzu wa Fasihi

Fasihi Andishi

Mifano

  • Mstahiki Meya
  • Kifo Kisimani
  • Shamba la Wanyama

Angalia

Hadithi Fupi

Riwaya

Tamthilia au tamthiliya ni sanaa ambayo huwasilisha mchezo wa kuigiza kwa njia ya maandishi. Majina ya wahusika huandikwa katika upande wa kushoto, kisha koloni, halafu hufuatiwa na maneno halisi yaliyotamkwa na mhusika huyo.

Aina za Tamthilia

Kunazo aina kadhaa za tamthilia katika fasihi andishi:

  1. Tamthilia Cheshi/Komedia – ni mchezo wa kuchekesha. Maudhui yake huundwa kwa lengo la kutumbuiza hadhira.
  2. Tamthilia Simanzi/Trejedia – ni mchezo uliojaa huzuni, mikasa, mikosi, visa vya kutisha na aghalabu baadhi ya wahusika wakuu hufa.
  3. Tamthilia Simanzi-Cheshi/Trejikomedia – ni mchezo wenye visa vya kuhuzunisha lakini pia unawasilisha kwa njia ya kuchekesha. Aghalabu wahusika hutumia kejeli kuchekesha hadhira ijapokuwa kuna shida fulani inayowakabili. Baadhi ya wahusika wakuu hukumbwa na mikasa.
    Mfano: Kifo Kisimani (na Kithaka Wa Mberia)
  4. Tamthilia Tatizo – ni mchezo wa kuigiza ambapo wahusika huwa na tatizo/shida kuu wanalotaka kulitatua. Tamthilia hii aghalabu hutumia mbinu ya taharuki ili kuwafanya hadhira wawe makini ili kuona jinsi tatizo hilo litakavyoishia.
  5. Tamthilia ya Domestiki Drama – ni mchezo unaoangazia maisha ya kawaida ya watu kama vile familia, urafiki, ndoa n.k
  6. Tamthilia ya Melodrama – ni mchezo ambao husisitiza sifa za wahusika kwa kuunda wahusika kuunda wahusika wenye sifa zilizopigiwa chuku na zisizobadilika. Tamthilia hizi huundwa kwa namna inayowafanya hadhira wawapende wahusika fulani na wawachukie wahusika wengine. Kwa mfano:
    • Shujaa ambaye hushinda kila mara
    • Wahusika wabaya ambao hubakia wabaya kutoka mwanzo hadi mwishi
    • Wahusika wazuri ambao hufanya vitendo vizuri kutoka mwanzo hadi mwisho
    • Wapenzi ambao hata wakitenganishwa bado watapendana
    • Aghalabu huishia kwa raha mustarehe

Mifano ya Tamthilia

  1. Kifo Kisimani
  2. Shamba la Wanyama
  3. Mstahiki Meya

Aina za MashairiZifuatazo ni aina za mashairi kulingana

Aina za Mashairi

Zifuatazo ni aina za mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika kila ubeti

AINA

#MISHORORO

MFANO

Umoja/tathmina

1

Tathnia

2

Tathlitha

3

Tarbia

4

Takhmisa

5

Tasdisa

6

Usaba

7

Ukumi

10

Tanbihi: Aina za Mashairi ni tofauti na Bahari za Ushairi. Aina za mashairi huzingatia idadi ya mishororo katika kila ubeti ilhali Bahari za Shairi hutegemea na muundo wa shairi kwa kuzingatia vina, mizani, vipande na mpangilio wa maneno. Shairi moja haliwezi kuwa la aina mbili (k.v tarbia na takhmisa) lakini shairi linaweza kuwa katika bahari zaidi ya moja.

Bahari za Ushairi

 Ushairi • Bahari za Ushairi

Bahari za ushairi ni nyingi sana. Shairi huainishwa katika bahari fulani kulingana na mtindo wake, umbo lake na matumizi ya lugha.

Baadhi ya bahari za ushairi ni:

  1. Utenzi – shairi ndefu lenye kipande kimoja katika kila mshororo.
  2. Mathnawi – ni shairi la vipande viwili (ukwapi na utao) katika kila mshororo.

Ewe mtunga silabi, na sauti ya kinubi,
Majukumu hatubebi, maadamu hatushibi,
Mateso kwa ajinabi, kwa mabwana na mabibi
Ukija hayatukabi, karibia karibia

  1. Ukawafi – ni shairi la vipande vitatu (ukwapi, utao na mwandamo) katika kila mshororo.

Nashindwa nikupe nini, nishukuru kwa malezi, mapenzi na riziki,
Ni pendo kiasi gani, lishindalo la mzazi, kweli mama hulipiki,
Ulinilinda tumboni, ukilemewa na kazi, ila moyo huvunjiki,
Kanilisha utotoni, mavazi pia malazi, ukitafuta kwa dhiki.

  1. Mavue – Shairi la vipande vinne (ukwapi, utao, mwandamo na ukingo) katika kila mshororo.

Sisi walipa ushuru, wajenga taifa, tena kwa bidii, twahangaishwa,
Tumenyimwa uhuru, tuna mbaya sifa, hatujivunii, tunapopotoshwa,
Kila tunapopazuru, damu na maafa, hatutulii, hali ya kutishwa

  1. Ukaraguni – shairi ambalo vina vyake vya kati na vya mwisho hubadilika kutoka ubetio mmoja hadi mwingine.

Vina Ubeti 1: —ni, —mi,
ubeti 2: —ta, —lo,
ubeti 3: —po, —wa,

  1. Ukara – shairi ambalo vina vya kipande kimoja havibadiliki kutoka ubeti mmoja hadi mwingine, lakini vina vya kipande kingine hubadilika. Kwa mfano, vina vya kati vinafanana kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho lakini vina vya kipande cha mwisho vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.

vina Ubeti 1: —shi, —ma,
ubeti 2: —shi, —ko,
ubeti 3: —shi, —le,
ubeti 4: —shi, —pa

  1. Mtiririko – shairi ambalo vina vyake vya mwisho na vya kati havibadiliki kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho.

kwa mfano vina vikiwa ( —ni, —ka) kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho.

  1. Mkufu/pindu – Shairi ambalo neno la mwisho au kifungu cha mwisho cha maneno katika ubeti mmoja, hutangulia katika ubeti unaofuatia.

Hakika tumeteleza, na njia tumepoteza,
Nani wa kutuongoza, aliyepewa uweza,
Filimbi akipuliza, tusiyeweza kupuuza,
Bali twaisikiliza, bila ya kuzungumza,

Bila ya kuzungumza, wala mwendo kulegeza,
Tumwandame ja mwangaza, kututoa palipo giza,
Penye dhiki ya kuliza, bila sauti kupaza
Pengo hili kulijaza, ni nani anayeweza,

  1. Kikwamba – Neno moja au kifungu cha maneno hurudiwarudiwa kutanguliza mishororo au ubeti katika shairi.

Jiwe hili lala nini, ila moshi na majani,
Jiwe linalala lini, litokapo vileoni,
Jiwe hili halineni, lina macho halioni,
Jiwe na tulibebeni, tulitupe mitaroni

  1. Kikai – Shairi lenye kipande kimoja kifupi (chenye mizani chache kuliko kingine) Mfano (8,4)

Nani binadamu yule, adumuye,
Anayeishi milele, maishaye
Jenezani asilale, aluliye,
Kaburi liko mbele, sikimbiye.

  1. Msuko – Shairi ambalo kibwagizo/mshororo wa mwisho ni mfupi kuliko mishororo mingineyo. K.v (8,8) (8,8) (8,8) (8).

Hawajazawa warembo, usidhani umefika,
Ukisifiwa mapambo, jinsi ulivyoumbika,
Akipata jipya umbo, ‘tabaki kihangaika,
Usidhani umefika.

  1. Mandhuma – shairi ambalo kipande kimoja hutoa hoja, wazo ama swali, huku cha pili kikitoa jibu/suluhisho.
  2. Malumbano – Mashairi mawili ambapo mshairi mmoja hutunga shairi akijibu au kupinga utunzi wa mshairi mwengine.
  3. Ngonjera – Shairi lenye wahusika wawili wanaojibizana. K.m. Ubeti wa kwanza, mwalimu, na wa pili, mwanafunzi.
  4. Sakarani – Shairi lenye bahari zaidi ya moja.
  5. Sabilia – Shairi lisilokuwa na kibwagizo. Kituo (mshororo wa mwisho) hubadilika kutoka ubeti hadi ubeti.
  6. Shairi huru – shairi lisilozingatia sheria za ushairi
  7. Shairi guni – shairi lenye makosa ya arudhi za shairi

Uchambuzi wa Mashairi

FasihiUshairi • Uchambuzi wa Mashairi

Yafuatayo ni mambo muhimu unayohitajika kuzingatia kila unapochambua shairi.

  1. Muundo/Umbo la shairi
  2. Uhuru wa Mshairi
  3. Maudhui
  4. Dhamira
  5. Mtindo wa / Mbinu za Lugha

1.      Muundo/Umbo la Ushairi

Katika umbo wa shairi, tunaangazia jinsi shairi lilivyoundwa kwa kuangazia mizani, vina, mishororo n.k Aidha, ni muhimu kutaja aina na bahari za shairi zinazohusiana na kila sifa uliyoitaja.

    1. Idadi ya mishororo katika kila ubeti – Tumia idadi ya mishororo kubainisha aina ya shairi hilo.
      Kwa mfano: Shairi lina mishororo minne katika kile ubeti, kwa hivyo ni Tarbia
    2. Idadi ya mizani katika kila mshororo na katika kila kipande cha mshororo.
      Kwa mfano: Kila mshororo una mizani kumi na sita: nane katika utao na nane katika ukwapi.
    3. Idadi ya vipande katika kila mshororo – Taja ikiwa shairi lina kipande kimoja, viwili, vitatu au vinne kisha utaje bahari yake.
    4. Kituo, kiishio au kibwagizo – Ikiwa mstari wa mwisho umerudiwa rudiwa, basi shairi lina kibwagizo au kiitikio, la sivyo lina kiishio.
    5. Vina – Zingatia vina vya kati na vya mwisho kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Kisha utaje ikiwa ni Mtiririko, Ukara au Ukaraguni

2.      Uhuru wa Mshairi

Mshairi hafungwi na kanuni za kisarufi za lugha katika utunzi wa shairi. Anaweza kufanya makosa ya kisarufi kimakusudi ili shairi lizingatie umbo fulani. Zifuatazo ni njia mbalimbali ambazo mtunzi wa shairi anaweza kutumia kuonyesha uhuru wake.

    1. Inkisari – kupunguza idadi ya silabi katika neno ili kusawazisha idadi ya mizani katika mshororo.
      mfano: kubadilisha ‘nimeona aliyenipenda‘ kuwa ‘meona alenipenda‘.
    2. Mazda – kuongeza silabi katika neno ili kusawazisha idadi ya mizani katika mshororo.
      mfano: afya ukijaliwa kuwa afiya ukijaliwa .
    3. Tabdila – kubadilisha silabi ya mwisho ili kustawazisha urari wa vina katika kipande bila kuathiri mizani.
      mfano: yahuzunisha dunia kuwa yahuzunisha duniya .
    4. Kuboronga Sarufi -ni mbinu ya kupangua mpangilio wa maneno ili kuleta urari wa vina au mdundo wa ushairi.
      mfano: siku hiyo ikifika kuwa ikifika hiyo siku .
    5. Utohozi – Kuswahilisha Maneno – Wakati mwingine mshairi anaweza kubadilisha neno la lugha nyingine litamkike kwa Kiswahili ili kudumisha mdundo wa kishairi na pia kupata neno mwafaka litakalotimiza arudhi za kiushairi.
      mfano: tukapata intaneti badala ya tukapata ‘internet’ ama mtandao wa tarakilishi.

3.      Maudhui

Maudhui ni jumla ya ujumbe na mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika shairi fulani. Haya ni mambo yanayotajwa katika hadithi na yanaweza kujumuisha mawazo zaidi ya moja. Maudhui husaidia kujenga dhamira ya shairi.

4.      Dhamira

Dhamira ni lengo, dhumuni au nia ya mtunzi wa shairi. Mtunzi wa shairi anaweza kuwa na kusudi la kutuonya, kututahadharisha au kutunasihi kuhusiana na jambo fulani.

5.      Mtindo wa Lugha

Mtindo wa lugha hurejelea namna mbalimbali ambazo mshairi anatumia mbinu za lugha. Mshairi anaweza kutumia mbinu za lugha. kama vile: Tanakali za Sauti, Istiara, Takriri, Semi n.k

the islamic religious education

Definition of Islam

The term Islam has several meanings

  • Submission and obedience
  • Peace
  • Cleanliness

SUBMISSION AND OBEDIENCE

To submit is to put something forward for consideration .e.g. a true Muslims should put Allah [s.w.t] forward for what he wants. i.e. one has to depend on Allah totally.

To obey is to do as told or commanded .A true Muslim should obey Allah [s.w.t] ‘s commandment i.e. Allah has command Muslims to establish swalah, give zakat and a void zinah by doing so shows obedient to Allah’s command

PEACE

A true Muslim should maintain peace with himself i.e. He should not commit suicide.muslims should also maintain peace with fellow human beings and to other creatures like ants, birds, insect est. that a Muslim should not kill anything except for just good reason and for leisure Muslim should maintain peace with his lord by obeying His commandments.

CLEANLINESS/PURITY

The prophet [s.w.a] said, Islam is cleanliness, “None shall enter paradise except the clean.”A Muslim should have a clean heart which will be recognized by him being kind, honest, generous, humble and always seen assisting the poor and the needy people. A Muslim should maintain cleanliness of his body, clothes and the place of ibadah e.g. swalah

DEVOTIONAL ACTS

Is based on the pillars of religion [arkanul diin] there are three pillars of religion:-

  • Pillars of islam
  • Pillars of imaan
  • pillar of ihsaan

PILLARS OF ISLAM

There are five pillars of Islam

  • shadah
  • swalah/prayer
  • zakat /alms
  • swaum/fasting
  • hajj/pilgrimage

PILLARS OF IMAAN [FAITH]

There are six pillars of imaan

  • to believe in Allah [s.w.t.]
  • to believe in his Angels
  • to believe in his holy books
  • believe in his prophet
  • to believe in his last day
  • to believe in Allah’s  qadha wal qadar[ goodness/excels and badness]

PILLARS OF ISLAM

1] SHAHADA

Words of shahada

ASH-HADU-AN-LAA—ILAAHA-ILA-LLAH-WA-ASH-HADU-ANAA-MUHAMDAN-RASULULLAH.

“I bear witness that there is no God worthy of praise and worship except Allah and I bear witness that Muhammad is the messenger “

IMPORTANCE OF SHAHADA

  • It is one of the pillars of Islam
  • Declaration of word of shahada changes Non-Muslim to be a Muslim
  • It recognizes ones of Allah [s.w.t.]
  • It prevent committing of Shirk
  • It recognizes Muhammad [s.a.w.]as a messenger of Allah [s.w.t.]
  • Declaration of the words of shahada increases faith
  • Whoever  recite the words  of shahada is rewarded by Allah [s.w.t.]

Tawheed

Means the oneness of Allah [s.w.t.] Or unity of Allah.

Words of Tawheed

“Laa-illaha-ila llah”

There is no God except Allah [s.w.t]

“Verily Allah loves those who fight in His cause arrayed in [solid] ranks, as though they are [strong] structure cemented with [molten] lead.” 51 We must never confuse the fields of Da’wah, Hisbah and Jihad. Each of these has its areas of action, rulings and circumstances which make one the only means to be used and not the others. It is a pity that many of those who work for Islam do not make a distinction between these areas. As a result of this, they employ harshness when the situation calls for kindness, or kindness when harshness is required. Some of them would engage in preaching on the Battlefield while others would wield the sword instead of practicing Da’wah. While doing this, they are either prompted by ignorance or motivated by personal desires. If they are prompted by ignorance, then this is a catastrophe; and if they are motivated by personal desires, this is a greater catastrophe. The second issue concerns those who actively work for the Islamic movement. They should be well aware of their duty in this world, their Da’wah and the grave responsibility which they alone carry. They should prepare themselves to practise Da’wah with all its requirements, namely knowledge, wisdom, clear argument, shrewdness, intelligence and understanding of the human self, its whims, diseases and remedies. They should also prepare themselves to practise Hisbah with all its requirements, namely knowledge, patience, endurance, determination and courage to stand up for the truth. They must also prepare themselves to undertake Jihad and arm themselves with everything this course requires: strength, fortitude, courage, sacrifice, training, preparation and expertise. The Islamic movement will surely fail to establish the religion of Allah on earth if it neglects to provide its members with this comprehensive education and contents itself with some aspects of Islam at the cost of others. To put it clearly, it is not enough that we become a group of preachers, good only at practicing Da’wah, forgetting, or trying to forget, that there are people who can be dissuaded from sin only by force, and regimes and sects which can only be swayed by the sword. At the same time, it is not enough that we should all turn into an army, taking up arms on every occasion and unable to practice Da’wah or undertake the religious education of the people, incapable of gentle persuasion, forgetting that with some people it suffices to merely caution or chide. It is utterly wrong to take up the sword where Da’wah and gentle persuasion is required and to undertake admonition and good counsel on the Battlefield. May Allah’s peace and blessings be upon the Prophet who observed all these commands. Allah says (which means): “O Prophet! Verily, We have sent you as a witness and a bearer of glad tidings; a warner and a summoner unto Allah by His command, and as a lamp that gives light.” [Surah Al-Ahzaab (33), Ayat 45-46.] “He enjoins on them good and forbids them evil.” [Surah Al-A’raaf (7), Ayah 157.] “Fight, therefore, in the cause of Allah.” [Surah An-Nisa (4), Ayah 84.] “Verily you have in the Prophet of Allah a beautiful example to follow for him who hopes in [the Meeting with] Allah and the Last Day and who remembers Allah much.” [Surah Al-Ahzaab (33), Ayah 21.]

Baklawa Za Pistachio Na LoziBiskuti   Vipimo Philo (thin pastry) manda

Baklawa Za Pistachio Na Lozi

Vipimo

Philo (thin pastry) manda nyembamba                            1 paketi                                                  

Siagi                                                                     ¼ Kikombe cha chai

Baking powder                                                        2 Vijiko vya chai

Pistachio/ lozi                                                          2 vikombe vya chai

Mafuta                                                                     ½ Kikombe

Shira

Sukari                                                                              2 Vikombe vya chai

Maji                                                                       2 ½ Vikombe vya chai

ndimu                                                                               ½ kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1.       Tafuta treya iliyokuwa sawa na ukubwa wa hizo manda nyembamba (philo) au zikate hizo manda kwa ukubwa wa treya (mraba au mstatili)

2.        Kisha yeyusha siagi changanya na mafuta.

3.        Kisha panga manda moja pakaza mafuta juu yake kisha weka manda nyingine juu yake kisha pakaza mafuta tena weka manda nyingine juu yake, endelea kufanya hivyo mpaka ziwe kama sita au saba kisha nyunyizia pistachio na lozi halafu panga tena manda na mafuta manda na mafuta tena sita au saba kisha nyunyizia tena pistachio na  lozi.

4.        Panga namna hivyo mpaka treya ijae inapofika manda ya mwisho kata vipande vya mraba vidogodogo humo humo kwenye treya kisha nyunyizia mafuta yaliyobaki.

5.        Washa moto wa oven 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi rangi ibadilike kidogo (isikauke sana)

6.        Chemsha syrup yako kama shira ya majimaji lakini isiwe nzito sana ikishakuwa tayari mwisho tia ndimu acha ipoe kidogo kisha miminia juu ya treya yote halafu malizia kunyunyizia pistachio na lozi zilizobaki.

7.       Zikishakuwa tayari zipange kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

Vidokezo:

Ukishatoa treya kwenye oven wacha ipoe kidogo na syrup yako pia wacha ipoe kidogo kabla hujamimina, ukitia ya motomoto zitalainika.

Manda nyembamba za baklawa zinauzwa tiyari madukani kwenye pakiti.